Dk. Munroe akiwa nchini Tanzania mwezi Oktoba mwaka huu.
KIONGOZI wa Bahamas Faith Ministries, Dk. Myles Munroe, mkewe Ruth na watu wengine saba wamefariki dunia katika ajali ya ndege jana huko Bahamas.
Katika ajali hiyo, ndege ndogo waliyokuwa wakisafiria iligonga winchi na kulipuka wakati ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Grand Bahama.
Dk. Munroe ambaye pia alikuwa mzungumzaji maarufu wa mambo ya uongozi na biashara duniani, Oktoba 21, mwaka huu alitoa somo kwa viongozi mbalimbali nchini katika mkutano wake mkubwa uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar.
Katika mkutano huo, Dk. Munroe kutoka Nassau, Bahamas, alifundisha mbinu za kuwafanya viongozi waweze kuchanganua mambo, kutimiza majukumu yao na hatimaye kufikia malengo makubwa ya kimafanikio ambayo yanaweza kuifanya nchi ipige hatua.
Dr. Myles Munroe amefariki akiwa na miaka 60 huku akiwa kwenye ndoa na mkewe kwa miaka 35 Ajali ya ndege hiyo inayosemekana ilikua na watu wengine 9 akiwemo Makamu wa Rais wa Bahamas Faith Ministries, mchungaji Richard Pinder watu wengine haijajulikana bado majina yao japo inasemekana alikuwemo mtoto wa kike wa Dr. Myles Munroe ndani ya ndege hiyo.
0 comments:
Post a Comment