FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA SHINIKIZO LA DAMU



Shinikizo la damu ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu.
Shinikizo la damu hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer
Shinikizo la damu husababishwa na nini?
Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:
1. Uvutaji sigara
2. Unene na uzito kupita kiasi
3. Unywaji wa pombe
4. Upungufu wa madini ya potassium
5. Upungufu wa vitamin D
6. Umri mkubwa
7. Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
8. Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin
Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini. Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti.
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes).
Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment