ITAZAME DUNIA YOTE KWA KUTUMIA GOOGLE EARTH

Google earth ni programu inayomwezesha mtumiaji kuangalia ramani, miundombinu, jiografia na mambo mengine duniani kwa kutumia mtandao. 

Kabla ya kuitwa google earth, programu hii ilijulikana kwa jina la Earth3D Viewer chini ya Kampuni ya KeyHole iliyokuwa inadhaminiwa na Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA). 


Picha zote zinazoonekana unapofungua programu hii huwa zinatolewa na shirika la mambo ya anga za juu la Marekani (NASA) na bila mtandao huwezi kupata picha yoyote. 


Kuna aina mbili ya programu za google earth; ile ya Google Earth na Google Earth Pro. Tofauti ni kwamba hii Google earth Pro ni ya kulipia, yaani inauzwa na inakuwezesha kupata mambo mengi zaidi ya hiyo ya kwanza. 


Programu hii inakuwezesha kuruka juu kuangalia dunia jinsi ilivyo, kutembelea maeneo mbalimbali ya dunia kuanzia mbuga za wanyama, viwanja vya michezo, majengo, barabara, mitaa na vitu vingine vingi. 
Google earth imesaidia katika mambo mengi hasa kwenye masuala ya uhandisi, kwani baadhi ya wahandisi wa barabara hawalazimiki kwenda porini kwa ajili ya kuchukua ramani au baadhi ya vipimo vya maeneo wanayotaka kuweka barabara. 


Kwa wale wageni wa maeneo wanaweza kutumia google earth kwa ajili ya kutengeneza ramani ya maeneo wanayopenda kutembelea kisha wanahifadhi kwenye vifaa vyao. 


Kama uliwahi kusikia mradi wa magari yatakayokuwa yanajiendesha yenyewe, programu kama google earth ndiyo inawezesha utendaji wa magari kama hayo na vifaa vingine vinavyojiendesha vyenyewe. 


Hata hivyo, Google earth kwa upande mwingine imekuwa chanzo cha migogoro kati ya mataifa hasa katika masuala yanayohusu mipaka. Pia kuna suala la CIA kukusanya taarifa za watu na vitu bila ya wahusika kujua. Hii ilifanyika sana wakati ule wa Earth3D Viewer. 


Hapa kwetu suala la google earth liliwahi kuleta mgogoro kidogo baada ya watu kutumia programu hiyo kuweka mipaka ya Ziwa Nyasa na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii kama vile ndiyo halisi kumbe haikuwa na ukweli wowote. 


Huko Marekani kwenyewe kipindi cha nyuma kidogo kuliwahi kuibuka kelele kutoka kwa mamlaka nyingine za usalama kutokana na programu hii kutoa ramani za maeneo mbalimbali kama viwanja vya ndege, kambi za jeshi na barabara. 


Kimsingi faragha za watu ni kitu kinacholeta shida katika matumizi ya programu hii. Wakati mwingine mtu anaweza kupiga picha ya jengo au nyumba ya mtu na kujua mengi.MWANANCHI
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment