UNDANI KUHUSU MTOTO ALIYETESWA NA MFANYAKAZI WA NDANI


Baada ya video ilioyosambaa katika mitandao mbali mbali mwishoni mwa wiki hii, ikimuonesha msichana wa ndani akitekeleza ukatili uliopitiliza kwa mtoto mwenye umri wa miaka miwili tu(bofya hapa kuitizama), Kumekuwa na taarifa za uzushi katika mitandao ya kijamii zinazodai kuwa mtoto huyo amefariki dunia, lakini hasha mapema Mama wa mtoto huyo aliyefahamila kwa jina moja la Anjela amethibitisha kuimarika kwa afya ya mtoto huyo, ambapo amethibitisha kuruhusiwa kutoka hospitali.

Katika tukio hilo ambalo lilivuta hisia za watu wengi na kuwashitua wengi, msichana huyo alionekana akimuadhibu mtoto huyo kwa kipigo kikali huku akimkanyaga kanyaga mtoto huyo kama faru mwenye hasira.

Taarifa zinasema baba wa mtoto huyo alishtukia mwendendo ya afya ya mtoto wake na kuamua kufunga kamera ili kupata picha ya kinachoendelea pale wazazi hao wanapokuwa nje ya nyumba yao, ndipo alopofanikiwa kulinasa tukio hilo ambalo nusura limsababishie kifungo, kufuatia kipigo kikali alichokitoa kwa msichana huyo wa kazi.

Hata hivyo taarifa zinasema kilichomsaidia ni ushahidi wa video hiyo ambayo hata maafisa wa usalama waliona alichokifanya kilikuwa haki tupu.

Msichana huyo wa kazi hali yake ni mbaya sana hivi sasa akila kwa kutumia mpira huku akikabiriwa na mkono wa sheria kwa kosa ka kufanya jaribio la mauaji.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment